03. Ukuu wa akili ni kutambua matukio kabla hayajatokea

1- Ukuu wa akilii ni kutambua matukio yaliyo njiani kabla hayajatokea.

2- Ni wajibu kwa mwenye busara kujiepusha na mambo matatu yanayoiharibu akili haraka kuliko moto unavyounguza majani makavu; kucheka kwa kipindukia, kuwa na matumaini mengi mabaya na mathibitisho mabaya.

3- Mwenye busara hujitolea kwa rafiki yake nafsi na mali yake, maarifa yake na uwepo wake na wema wake na ambaye si msomi bishara yake na mamkazi yake.

4- Aliye na busara hachukui msaada isipokuwa kwa yule anayejua kuwa atamsaidia. Hazungumzi isipokuwa tu na yule ambaye anaona maneno yake ni yenye faida isipokuwa kutapokuwa kuna dharurah ya kufanya hivo.

5- Fadhila za watu hazipatikani katika madai yao wenyewe. Zinapatikana katika yale watu wanayowanasibishia. Mwenye busara hajali mambo ya kidunia yaliyompita akilinganisha na ile akili aliyotunukiwa.

6- Aliye na busara hatamani kile asichokipata na wala halimbikizi pindi anapopata.

7- Mwenye busara anaheshimiwa pasi na pesa kama jinsi simba inavyoogopwa ingawa imelala.

8- Maneno ya mwenye busara ni ya sawa kama mwili wa aliye na afya njema na maneno ya mjinga ni yenye kujigonga kama mchanganyiko kwenye mwili wa mgonjwa.

9- Hata kama maneno ya mwenye busara yatakuwa mafupi, ni yenye thamani kubwa. Hata kama machafu ya mtenda dhambi ni madogo, ni msiba wa wazi.

10- Ni katika busara mtu kuthibitisha kwanza kabla ya kufanya kitendo chochote.

11- Ugonjwa wa busara ni kujiona. Ni juu ya mwenye busara kuwa na ustahamilivu kwa jirani muovu, jamaa waovu na matangamano maovu. Hatowaepuka jinsi siku zinavyokwenda.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 13/10/2016