Kuhusu ni nani ambaye anawajibika kufunga? Ni yule ambaye ´ibaadah inamuwajibikia kwa namna ya kwamba kumethubutu kwake sharti zifuatazo:

1 – Uislamu.  Kwa msemo mwingine ni kwamba swawm haisihi kutoka kwa kafiri katika hali ya ukafiri wake. Ikitokea amefunga, haisihi wala kukubaliwa kutoka kwake. Amesema (Ta´ala):

وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَبِرَسُولِهِ

”Haikuwazuilia kukubaliwa michango yao isipokuwa kwa kuwa wao walimkufuru Allaah na Mtume Wake.”[1]

Kafiri anazungumzishwa misingi ya ´Aqiydah kwa mujibu wa maafikiano ya wanazuoni[2]. Je, anawajibika pia na matawi ya Shari´ah? Wanazuoni wanatofautiana katika suala hili kwenye maoni mawili:

1 – Makafiri ni wenye kuzungumzishwa matawi ya Shari´ah na watafanyiwa hesabu kwa jambo hilo, jambo ambalo ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni[3]. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ

“Nini kilichokuingizeni katika [Moto wa] Saqar?” Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.”[4]

2 – Si wenye kuzungumzishwa matawi ya Shari´ah. Haya ni maoni ya Hanafiyyah (Rahimahumu Allaah)[5].

[1] 09:54

[2] al-Furuuq (01/222) na ”al-Ibhaaj” (01/176-177) ya as-Subkiy.

[3] Sharh Tanqiyh-ul-Fusuwl, uk. 162, ”al-Burhaan fiy Usuwl-il-Fiqh” (01/17) na ”Sharh Mukhtaswar-ir-Rawdhwah” (01/205).

[4] 74:42-43

[5] al-Ikhtiyaar lita´liyl-il-Mukhtaar (03/111).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/432-433)
  • Imechapishwa: 13/02/2025