Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, kufufuliwa baada ya mauti na kuamini makadirio; kheri yake na shari yake.

MAELEZO

Maneno yake:

“Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake… “

´Aqiydah yao ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho. Katika upokezi mwingine imekuja:

“Kuamini kufufuliwa baada ya mauti.”

Vilevile inatakiwa kuamini makadirio; kheri na shari yake. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah matawi yake yanatokana na misingi hii sita:

1 – Kumuamini Allaah.

Inaingia katika kumuamini Allaah kuamini vilevile kuwa Yeye ni Mmoja pekee, hali ya kuwa hana mshirika. Vilevile inatakiwa kuamini kuwa Allaah aliwatuma Mitume, akateremsha Vitabu, akaweka Shari´ah ya mambo mbalimbali. Humo kunaingia nguzo za Uislamu ambazo ni swalah, zakaah, swawm na hajj. Yote haya yanaingia katika kumuamini Allaah na kuamini kuwa Yeye ni Mmoja pekee na ´ibaadah anastahiki kufanyiwa Yeye pekee. Vilevile kuamini kuwa Yeye ndiye aliyeweka Shari´ah kama vile swalah, zakaah, swawm, hajj na hukumu nyenginezo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 12
  • Imechapishwa: 31/05/2023