2 – Malaika Wake.

Bi maana kuamini wale wote ambao Allaah amewataja katika Kitabu Chake au waliothibiti katika Sunnah sahihi. Ahl-us-Sunnah wanawaamini wote hao. Baadhi yao ni Jibriyl, Mikaaiyl, Israafiyl, Malaika wa mauti, mlinzi wa Moto na wengineo. Malaika waliotajwa kwa njia ya upambanuzi wanawaamini kiupambanuzi. Malaika waliotajwa kwa njia ya ujumla – kama mfano ya wabebaji wa ´Arshi wanaoitwa Kuruubiyyuun na wengineo – Ahl-us-Sunnah wanawaamini kiujumla. Wanaamini kuwa Allaah anao Malaika na miongoni mwao wako wanaobeba ´Arshi ambao ni Kuruubiyyuun, wanaotulinda, ambao wamepewa kazi ya kutuchunga, Jibriyl, Mikaaiyl, Israafiyl na wengineo. Tunawaamini wote na kwamba ni waja wa Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ

“Bali ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii kwa kauli nao kwa amri Yake wanafanya.” (21:26-27)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 12
  • Imechapishwa: 31/05/2023