Mtunzi wa kitabu amesema:

“Kinyume chake ni ukafiri.”

Endapo kafiri ataswali swalah yake haisihi. Hakuna kitendo chochote kinachokubaliwa na kusihi mpaka kijengeke juu ya Tawhiyd. Maneno yake:

“Matendo ya kafiri ni yenye kurudishwa, bila ya kuzingatia sawa akifanya ´amali yoyote ile.”

Akifunga funga yake haisihi na ni yenye kurudishwa. Akiwatendea wema wazazi wake wawili haisihi na ni yenye kurudishwa. Akiwaunga jamaa zake haisihi na ni yenye kurudishwa. Akipambana jihaad haisihi na ni yenye kurudishwa. Akiamrisha mema haisihi na ni yenye kurudishwa. Matendo ya kafiri hayasihi. Siku ya Qiyaamah ataadhibiwa kwa kuacha kwake Uislamu, swalah na zakaah.

Lakini analipwa juu ya matendo yake hapa duniani. Hivyo hupewa chakula kutokana na matendo yake aliyofanya kwa ajili ya Allaah hapa duniani. Halafu atakuja siku ya Qiyaamah akiwa hana mema yoyote na atumbukizwe Motoni. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume wa  Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hamdhulumu muumini kwa tendo jema alilofanya; analipwa duniani na analipwa Aakhirah. Kuhusu kafiri hulishwa kwa yale mema aliyofanya kwa ajili ya Allaah duniani mpaka atapoenda Aakhirah atakuwa hana mema yoyote atakayolipwa kwayo.”[1]

Kwa hivyo kafiri akifanya mema duniani basi hulishwa kwayo hapa duniani. Kwa hivyo anatangulia kuchukua malipo yake na anaenda Aakhirah pasi na kuwa na matendo yoyote. Tunamwomba Allaah usalama na afya.

[1] Muslim (2808).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 10
  • Imechapishwa: 06/12/2021