03. Kutawadha kwa maji yaliyochanganyikana na magugu na mchanga

Swali 03: Tulitoka kikosi cha watu kuelekea nchi kavu na tukaketi juu ya kijito cha maji. Maji yalikuwa yamezibwa kwa matope na baadhi ya mitishamba. Je, inafaa kutawadha kwa ajili ya swalah kwa maji haya[1]?

Jibu: Inafaa kutawadha kwa mfano wa maji haya, kuoga kwayo na kunywa kutoka humo. Kwa sababu bado yanaitwa maji. Ni masafi na ule udongo na magugu hayayaondoshi kutoka katika ile sifa yake ya usafi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/17).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 16/02/2022