04. Kula na kunywa ndani ya vyombo vya mayahudi na manaswara

Swali 04: Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kula ndani ya vyombo vya mayahudi na manaswara isipokuwa katika hali ya dharurah. Hilo ni kwa sababu wanaweza kula ndani yake nyama ya nguruwe na wakanywa ndani yake pombe. Je, vyombo vya muislamu anayekunywa pombe ndani yake vina hukumu moja? Je, inafaa kutawadhia ndani yake[1]?

Jibu: Ikiwa anachelea kuweko ndani ya vyombo hivyo pombe au mabaki ya nguruwe, basi analazimika kuviosha akivihitaji kisha anywe ndani yake. Asipovihitaji basi himdi zote anastahiki Allaah. Kila chombo ambacho anakhofia kuweko najisi ndani yake – ni mamoja ni cha makafiri au cha wasiokuwa makafiri – anatakiwa kukiosha na kula ndani yake. Kama mfano wa alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msipopata vyengine basi viosheni na mle ndani yake.”[2]

Vivyo hivyo hapana neno kutawadha ndani yavyo baada ya kuviosha.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/23).

[2] al-Bukhaariy (5170) na Muslim (4960).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 15
  • Imechapishwa: 16/02/2022