03. Kuingiwa na hamu baada ya kusikia fadhila za elimu

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha kuwa kila kilichomo duniani hakina kheri isipokuwa vile vilivyovuliwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Dunia imelaaniwa na vimelaaniwa vilivyomo ndani yake isipokuwa kumdhukuru Allaah na vyenye maana kama hiyo, mwalimu na mwanafunzi.”[1]

Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote ya kwamba muislamu akisikia fadhila hizi basi moyo wake utatikisika, hamu yake itazidi kuwa kubwa na nafsi yake itapata uchangamfu wa kuitafuta elimu. Atapohisi hivo basi anatakiwa ajiandae kupita njia za Kishari´ah ambazo zimewekwa na Shari´ah katika kutafuta elimu.

[1] at-Tirmidhiy (2322), Ibn Maajah (4112). at-Tirmidhiy amesema: “Ni nzuri kutokana na zingine.” Kadhalika ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (2797).

Kujifunza elimu katika Uislamu kuna fadhila kubwa mno.

 

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016