03. Je, swalah ya Tarawiyh imesuniwa kwa watu watatu wanaoeshi mashambani?

Swali: Je, swalah ya Tarawiyh imesuniwa kwa watu watatu wanaoeshi mashambani?

Jibu: Ndio, inafaa kwa wale ambao pambizoni mwao hakuna msikiti ambapo wanaweza kuswali ndani yake wakaswali Tarawiyh hata kama watakuwa wawili, watatu au wane. Bali kama atakuwa mmoja inafaa kwake kufanya hivo. Kwa sababu Tarawiyh ni kusimama katika Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesimama [nyusiku za] Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio basi atasamehewa dhambi zake zilizotangulia.”[1]

[1] al-Bukhaariy (37) na Muslim (759).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 08-09
  • Imechapishwa: 09/04/2022