Swali: Baadhi ya vijana hawafungi pamoja na wananchi wao katika miji yao. Wanadai kuwa nchi zetu hazifuati Shari´ah na kwa ajili hiyo wanaamua kuifuata Saudi Arabia.

Jibu: Ikiwa hakuna juu yao madhara au hawaleti mpasuko wa mkusanyiko, basi ni jambo zuri. Lakini kunakhofiwa endapo mtu atafunga kivyake na akatangaza funga yake atasababisha mpasuko. Ikiwa hakukhofiwi jambo hilo, basi hapana shaka ni vizuri kufunga na wengine. Lakini mtu anatakiwa apupie kusiwepo mpasuko na magomvi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 17/03/2022