Swali: Ni ipi hukumu ya kufunga Ramadhaan kwa ambaye haswali?

Jibu: Swalah ndio nguzo muhimu zaidi katika Uislamu baada ya Tawhiyd. Ambaye haswali, nakhofia isikubaliwe funga yake. Kwa sababu kikosi cha wanazuoni wanaona kuwa kuacha swalah ni ukafiri. Kwa ajili hiyo sionelei usahihi wa swawm ya ambaye haswali. Swalah ni muhimu zaidi kuliko funga.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 17
  • Imechapishwa: 17/03/2022