Swali: Je, nalazimika kutia nia kila siku ya Ramadhaan ninayofunga au inatosha kutia nia moja pale mwanzoni mwa mwezi?

Jibu: Mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhaan muislamu atie nia ya kufunga mwezi mzima. Isipokuwa akilazimika kuvunja swawm yake kwa sababu ya safari, ugonjwa na mfano wake. Vinginevyo kimsingi muislamu anaweza kuweka nia mwanzoni mwa mwezi ya kufunga Ramadhaan nzima. Kila usiku wa Ramadhaan anaihudhurisha moyoni mwake. Hapana shaka kwamba anakuwa tayari kula daku na kufunga.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 17
  • Imechapishwa: 17/03/2022