02. Hesabu za astronomia za Ramadhaan kwa ajili ya mwezi mwandamo

Swali: Ufaransa tunayo kamati ambayo husimamia suala la kutangaza kuingia kwa Ramadhaan inasema waziwazi kuwa inategemea hesabu za astronomia, jambo ambalo hulithibitisha katika tovuti yake rasmi. Je, tuwafuate?

Jibu: Kimsingi ni kuwa kila muislamu anafunga na nchi yake. Ikiwa watu wa nchini mwake wako namna hiyo afanye nini? Vinginevyo ukweli wa mambo Saudi Arabia ndio inayotakiwa kufuatwa kwa sababu ndio nchi pekee inayothibitisha kuanza na kumalizika Ramadhaan na Dhul-Hijjah kwa njia inayokubalika katika Shari´ah. Saudi Arabia inatendea kazi Shari´ah inapokuja katika suala la mwezi mwandamo kwa ajili ya kuigiliza maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fungeni mtakapouona na fungueni mtakapouona.”[1]

Lakini yule aliyeko katika nchi na anachelea kugawanyika kwa watu wake basi huyu ameghilibiwa katika jambo lake.

[1] al-Bukhaariy (1900) na Muslim (1080).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 16
  • Imechapishwa: 17/03/2022