03. Chunga moyo wako usije kupigwa muhuri

Enyi waislamu! Ni lazima kwetu kutahadhari na kujifananisha huku. Ni lazima kwa muislamu kutilia umuhimu ijumaa na aikimbilie. Imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Wakome watu kuacha [swalah za] ijumaa au atazipiga muhuri nyoyo zao kisha watakuwa miongoni mwa waghafilikaji.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Moyo wake ukipigwa muhuri na akawa miongoni mwa waghafilikaji, basi anaangamia. Amesema (Ta´ala):

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

“Allaah amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao na juu ya macho yao pana kifuniko na watapata adhabu kuu.”[2]

Hii inafahamisha kwamba yeyote ambaye atachukulia wepesi amri ya Allaah na akapoteza yale ambayo Allaah amemuwajibishia, basi kuna khatari akapigwa muhuri juu ya moyo na masikizi yake na kukawekwa vizibo juu ya macho yake. Hatimaye hawi mwenye kuongoka kuifuata haki na haioni. Kwa hivyo inapata kueleweka kwamba swalah ya ijumaa jambo lake ni kuu na kwamba ni khatari kuichukulia wepesi.

[1] Muslim (1432) na an-Nasaa´iy (1353).

[2] 02:07

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 47
  • Imechapishwa: 29/11/2021