Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

na akufanye ni mbarikiwa popote utapokuwa.

MAELEZO

Bi maana akufanye ni mwenye kubarikiwa popote utapokuwa katika matendo yako, katika kuwanufaisha watu, katika nafasi yako na katika uombezi. Kwa msemo mwingine katika kila kitu.

Mtu aliyebarikiwa ni yule ambaye manufaa yake yanaenea kwa wengine katika kuwalisha wenye njaa na kubeba mazito yao na kuwasaidia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 118
  • Imechapishwa: 03/03/2023