Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ninamuomba Allaah Mkarimu, Mola wa ´Arshi tukufu, akuhifadhi duniani na Aakhirah,

MAELEZO

Ameanza kitabu hiki kwa du´aa. Hii ni namna ambavyo imamu huyu (Rahimahu Allaah) anawatakia watu kheri ambapo anakufunza na pia anakuombea du´aa.

Amefanya Tawassul kwa Allaah kutokana na utukufu na uola Wake juu ya ´Arshi ambayo ndio kiumbe kilicho juu zaidi na kwa jina Lake tukufu. Amekuombea Allaah akuhifadhi, ee mwanafunzi, duniani na Aakhirah na akuwafikishe katika yale yenye manufaa na dunia na Aakhirah yako. Ambaye anahifadhiwa na Allaah duniani na Aakhirah hupata furaha ambayo hakuna kula khasara baada yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 117
  • Imechapishwa: 03/03/2023