01. Utangulizi wa “Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah”

Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee mja na Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Amma ba´d:

Tunamshukuru Allaah kuweza kuzungumzia “al-Qawaa´id al-Arba´ah” ya Imaam na al-Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Ni chenye umuhimu mkubwa sana. Kwa sababu kimepambanua kati ya Tawhiyd na shirki. Kimeitwa “al-Qawaa´id al-Arba´ah” kwa sababu kimekusanya kanuni nne ambazo kwazo anapambanuka muumini na kafiri, mshirikina na mpwekeshaji. Dalili zake zimechukuliwa kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah.

Tunamuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) atufanye kuwa miongoni mwa wanaomwabudu Yeye pekee na wanaomtakasia nia, atuthibitishe juu ya uongofu na awaongoze waislamu waliopotea.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah na watakaowafuata.

Imeandikwa;

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 115
  • Imechapishwa: 03/03/2023