Ndugu! Mada ya muhadhara wetu huu “Zaad daa´iyah ila Allaah”. Zawadi ya kila muislamu ni ile ambayo Allaah ameibainisha pale aliposema:

وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ

“Chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu nikumcha Allaah.”[1]

Zawadi ya kila muislamu ni uchaji wa Allaah (´Azza wa Jall) ambao ameutaja kwa kukariri ndani ya Qur-aan hali ya kuiamrisha, kuwasifu wanaotekeleza, kubainisha thawabu zake na mengineyo katika njia za maneno:

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ

“Kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah. Ambao wanatoa katika hali ya wasaa na katika hali ya dhiki na wanajizuia ghadhabu na wenye kuwasamehe watu. Na Allaah anapenda wafanyao wema. Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao, basi humtaja Allaah wakaomba msamaha kwa madhambi yao – na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah? Na wasiendelee katika waliyoyafanya ilihali wao wanajua. Hao malipo yao ni msamaha kutoka kwa Mola wao na mabustani yapitayo chini yake mito hali ya kuwa ni wenye kudumu humo – na uzuri ulioje ujira wa watendaji!”[2]

Pengine mkauliza uchaji Allaah ni kitu gani? Jawabu ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Twalq bin Habiyb (Rahimahu Allaah) ambaye amesema:

“Uchaji ni kule kutenda kwa kumtii Allaah, juu ya nuru ya Allaah hali ya kutarajia thawabu.”

Katika maneno haya amekusanya kati ya elimu, matendo, kutarajia thawabu na kuogopa adhabu. Huu ndio uchaji.

Sote tunatambua kwamba yule anayelingania katika dini ya Allaah ndiye mtu ambaye ana haki zaidi ya kujipamba kwa tabia hii ambayo ni kumcha Allaah. Anatakiwa kufanya hivo kwa ndani na kwa nje. Kutokana na msaada wa Allaah (´Azza wa Jall) nitakumbusha katika mnasaba huu yale yanayohusiana na mlinganizi na yale anayopasa kujifanyia akiba na zawadi:

[1] 02:197

[2] 03:133-136

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaad Daa´iyah ila Allaah, uk. 10
  • Imechapishwa: 28/10/2021