02. Wasifu wa mtunzi wa kitabu Ibn Abiy Daawuud

Anaitwa Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud Sulaymaan bin Ash´ath as-Sijistaaniy.

Baba yake ni Abu Daawuud Sulaymaan bin Ash´ath ambaye ni mmoja katika wale watunzi wa vitabu vya Sunan vinne ambavyo ni muhimu.

Abu Daawuud ni katika maswahiba na wanafunzi wa Imaam Ahmad. Ana maswali aliyopokea kutoka kwa Imaam Ahmad yaliyochapishwa kwa jina “Masaa-il Abiy Daawuud”.

Mtoto wake huyu mtunzi anaitwa ´Abdullaah. Kun-ya yake ni Abu Bakr. Ni imamu mtukufu. Alisoma kwa baba yake na kwa wanazuoni wengine waliokuwa wakati wake. Alikuwa amebobea katika elimu, mapokezi na akasimulia. Ni mtu ambaye ana nafasi kubwa katika elimu. Haitofautiani na nafasi aliokuwa nayo baba yake (Rahimahumaa Allaah) au inakaribia. Yeye ndiye ametunga mashairi haya yaliyo na ´Aqiydah ya Salaf.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 16/12/2023