Imani ni maneno, matendo, nia na kushikamana barabara na Sunnah.

Imani inazidi na kushuka.

Ilikuwa ni mwenendo wa wanazuoni kufanya uvuaji (الاستثناء) katika imani.

Mtu akiulizwa kama yeye ni muumini, basi anatakiwa kujibu kuwa ni muumini Allaah akitaka au anataraji kuwa ni muumini. Anaweza vilevile kusema kuwa anamwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Yake.

Yeyote atakayedai kuwa imani ni maneno pasi na matendo, basi huyo ni Murj´iy.

Yeyote atakayedai kuwa imani ni maneno na matendo ndio Shari´ah, basi huyo ni Murj´iy.

Yeyote atakayedai kuwa imani haizidi na wala haipungui, basi huyo ni Murj´iy.

Yeyote atakayesema kuwa imani inazidi na wala haipungui, basi amesema maoni ya Murji-ah.

Asiyeona kufanya uvuaji katika imani, basi huyo ni Murj´iy.

Yeyote mwenye kudai kuwa imani yake ni kama imani ya Jibriyl au ya Malaika, huyo sio Murji-ah peke yake; ni mbaya zaidi – ni mwongo.

Yule mwenye kudai kwamba watu hawatofautiani katika imani, amesema uwongo.

Yeyote atakayedai kuwImaam Harb bin Ismaa´iyl al-KirmaaniyImaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniya utambuzi wa moyo unanufaisha ijapokuwa mtu hakuzungumza, basi huyo ni Jahmiy.

Yeyote atakayedai kuwa ni muumini mbele ya Allaah na mwenye imani kamili, hii ndio aina mbaya kabisa ya Murji-ah.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 35-39
  • Imechapishwa: 23/05/2022