01. ´Aqiydah moja pekee ndio yenye kukubaliwa

Abul-Qaasim amesema: Abu Muhammad Harb bin Ismaa´iyl ametuhadithia:

Hii ni ´Aqiydah ya maimamu wa elimu, Ahl-ul-Athar na Ahl-us-Sunnah, wanaotambulika na kufuatwa kwayo – kuanzia kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka hii leo. Wale wanazuoni niliokutana nao huko ´Iraaq, Hijaaz, Shaam na kwenginepo wako juu yake. Yeyote anayekwenda kinyume na I´tiqaad hizi, akawachafua au akawakosoa wenye nayo, basi huyo ni mzushi ambaye ameacha Mkusanyiko na amepinda kutokamana na mwenendo wa Sunnah na njia ya haki.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 23/05/2022