02. Swali na utoe zakaah ili uingie Peponi

4 – Ibn Fudhwayl ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa Saalim bin Abiyl-Ja´d, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

”Bedui mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Amani ya Allaah iwe pamoja nawe, ee kijana wa Banu ´Abdil-Muttwalib!” Akasema: ”Kwako pia!” Bedui yule akasema: ”Mimi ni kutoka katika wajomba zako wa Banuu Sa´d bin Bakr na mimi ni mjumbe wa watu wangu. Nataka kukuuliza na baadaye nitayatangaza maswali niliyokuuliza, na nitakuomba na baadaye nitayatangaza maombi niliyokuomba.” Akasema: ”Jichukulie, ee ndugu wa Banuu Sa´d.” Akasema: ”Ni nani aliyekuumba na ni nani Muumba wa waliokuwa kabla yako na ni nani Muumba wa wataokuja baada yako?” Akasema: ”Allaah.” Akasema: ”Nakuuliza kwa jina la Allaah; Yeye ndiye aliyekutuma?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: ”Ni nani aliyeziumba mbingu saba na ardhi saba na kupitisha kati yavyo riziki?” Akasema: ”Allaah.” Akasema: ”Nakuuliza kwa jina la Allaah; Yeye ndiye kakutuma?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: ”Sisi tunapata katika Kitabu chako na wajumbe wako wanatuamrisha kuswali mchana na usiku swalah tano ndani ya nyakati zake husika. Nakuuliza kwa jina la Allaah; Yeye ndiye kakuamrisha?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: ”Sisi tunapata katika Kitabu chako na wajumbe wako wanatuamrisha tuchukue ngamia wetu wadogo na tuwape mafukara wetu. Nakuuliza kwa jina la Allaah; Yeye ndiye kakuamrisha?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: ”Sifikirii kukuuliza jambo la tano, wala silihitaji sana.” Kisha akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye amekutumiliza kwa haki! Mimi na wale watakaonitii katika watu wangu tutayafanyia kazi.” Halafu akarejea. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka yakaonekana magego yake na akasema: ”Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Akiwa mkweli basi ataingia Peponi.”[1]

[1] Swahiyh. Wapokezi wake wote ni wanamme wa al-Bukhaariy. Kuna ambayo inaitia nguvu kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Anas na itakuja baada yake.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 05/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy