Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa kwanza

Lengo ka kutumwa Mitume (´alayhimus-Salaam)

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

MAELEZO

Allaah – Ni jina la Allaah (Jalla wa ´Alaa) pekee ambalo linafuatiwa na majina mengine yote. Allaah (Ta´ala) amesema:

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ للَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ

Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu katika viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Allaah ambaye ni Vyake pekee vyote viliyomo katika mbingu na katika ardhi. Na ole kwa makafiri kutokana na adhabu kali.” (14:01-02)

Hatusemi kuwa neno la kitukufu ”Allaah” ni sifa, isipokuwa hali ya kubainisha. Neno la kitukufu linakuwa na maana ya sifa yenye kufuata kwa kile kinachosifiwa.

Jina – Mtunzi (Rahimahu Allaah) ameanza kitabu chake kwa Jina la Allaah kwa kuiga Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) kilichoanzwa kwa Basmalah. Kadhalika amefanya hivo kwa kufuata Hadiyth. Vilevile amemuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuwa siku zote akianza barua zake kwa jina la Allaah.

Mwingi wa rehema [ar-Rahmaan] – Mwingi wa rehema ni katika majina maalum ya Allaah (´Azza wa Jall) na hivyo haliitwi mwingine. Mwingi wa rehma maana yake ni yule Mwenye kusifika na rehema kunjufu.

Mwenye kurehemu [ar-Rahiym] – Ni jina ambalo huitwa kwalo Allaah (´Azza wa Jall) na wengineo. Maana yake ni mwenye rehema zenye kuendelea. Pale ambapo Mwingi wa rehema, ambaye rehema Zake ni kunjufu, na Mwenye kurehemu, ambaye ni mwenye rehema zenye kuendelea, yanakuwa pamoja, maana yake inakuwa “Mwingi wa rehema anayemfikishia rehema Zake kwa yule anayemtaka katika waja Wake”. Allaah (Ta´ala) amesema:

يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَرْحَمُ مَن يَشَاءُ ۖ وَإِلَيْهِ تُقْلَبُونَ

“Anamuadhibu amtakaye na anamrehemu amtakaye na Kwake mtarudishwa.” (29:21)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 23/04/2022