Himdi zote njema anastahiki Allaah. Tunamhimidi, tunamuomba msaada na msamaha. Tunajilinda Kwake kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na yule mwenye kupotezwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana na mshirika, na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake – swalah na amani zimwendee yeye, kizazi chake na Maswahabah zake na wale wenye kuwafuata kwa wema mpaka siku hiyo ya mwisho.

Ama baada ya hayo;

Haya ni maelezo mafupi ya kitabu cha Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab “Kashf-ush-Shubuhaat”. Humo mtunzi wa kitabu ametaja karibu hoja tata kumi za washirikina. Ameziraddi kwa majibu bora kabisa yanayosapotiwa na dalili, maana nyepesi na ibara za wazi. Ninamuomba Allaah (Ta´ala) amlipe thawabu kwa hilo na awanufaishe waja wa Allaah kwacho – hakika Yeye juu ya kila jambo ni muweza.

Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 11
  • Imechapishwa: 23/04/2022