Wale wanaotofautiana nasi wanaona kuwa imani ni maneno pasi na matendo. Kwa mtazamo wetu huyu ni mwenye kujigonga, kwa sababu akimaanisha kuwa ni maneno, basi ametambua pia kuwa ni matendo. Hajui kile nilichokufunza, kwamba waarabu wanayaita matendo ya viungo kuwa ni matendo. Hayo yanasadikishwa na Qur-aan inayotilia mkazo matendo ya moyo na matendo ya ulimi:

 إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ

“… isipokuwa yule aliyetenzwa nguvu na huku moyo wake umetua juu ya imani.”[1]

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا

“Ikiwa wawili nyinyi mtatubia kwa Allaah, basi hakika nyoyo zenu zimeelemea.”[2]

الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ

“… ambao anapotajwa Allaah basi nyoyo zao zinajaa khofu.”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kwenye mwili kuna kipande cha nyama; kinapotengemaa basi hutengemaa mwili mzima, na kinapoharibika basi huharibika mwili mzima. Nacho ni moyo.”[4]

Ikiwa mara moyo huwa ni wenye utulivu, wakati mwingine unapinda, mara nyingine unaogopa kisha wakati mwingine unatengemaa na kuharibika, inatosha kuonyesha matendo yake mengi. Baada ya hapo akabainisha maneno Yake msimamo wetu tuliosimamia:

وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ

“… na wanasema katika nafsi zao mbona Allaah hatuadhibu kwa yale tunayoyasema?”[5]

Haya yanafahamisha matendo ya moyoni.

[1] 16:106

[2] 66:4

[3] 22:35

[4] al-Bukhaariy (52) na Muslim (1599).

[5] 58:8

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 26/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy