Miongoni mwa dalili zinazofahamisha ubaya wa kutengeneza picha ni Hadiyth kama:
“Hakika Malaika hawaingii ndani ya nyumba yenye kinyago.”[1]
Kadhalika zipo Hadiyth nyingine nyingi ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasisitiza ubaya huo. Miongoni mwazo ni ile aliyoipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh), kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Jibriyl (´alayhis-Salaam) alinijia akasema: ”Nilikuwa nimekujia jana usiku. Hakuna kilichonizuia kuingia ndani ya nyumba uliyokuwemo isipokuwa ni kwamba kulikuwa na kinyago cha sanamu cha mwanamme. Katika nyumba kulikuweko kinyago cha sanamu katika pazia. Amrisha kichwa cha kinyago hicho kikatwe kiwe na umbile kama la mti. Amrisha pazia ikatwe na kufanywe mito miwili inayokanyagwa chini. Amrisha mbwa atolewe nje.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya hivo. Mbwa huyo alikuwa ni kilebu cha al-Hasan na al-Husayn kilichokuwa chini ya kitanda chao.”[2]
Swahiyh kwa mujibu wa at-Tirmidhiy.
´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiacha kitu chenye misalaba ndani ya nyumba yake isipokuwa anakivunja.”[3]
Ameipokea al-Bukhaariy na Abu Daawuud.
Abu Twalhah al-Answaariy ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Malaika hawaingii nyumba yenye mbwa wala picha ya sanamu.”[4]
Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy, Abu Daawuud na Ibn Maajah.
´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Malaika hawaingii nyumba yenye picha, mwenye janaba na wala mbwa.”[5]
Ameipokea Abu Daawuud na an-Nasaa´iy. Katika cheni ya wapokezi yumo ´Abdullaah bin Lahiy´ah ambaye ndani yake kuna udhaifu.
Abu Daawuud amesimulia kutoka kwa Safiynah, aliyesema:
”´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alimwalika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye chakula alichotengeneza. Alipokuja akaona pazia lenye mapambo akageuka na kurudi. Alipoulizwa juu ya hilo akasema: “Haifai kwa Nabii kuingia nyumba iliyopambwa sana.”[6]
[1] al-Bukhaariy (3322) na Muslim (2106).
[2] Abu Daawuud (4158). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Aadaab-uz-Zifaaf”, uk. 119.
[3] al-Bukhaariy (5949), Muslim (4151) na Abu Daawuud (4151).
[4] al-Bukhaariy (5949) na Muslim (2104).
[5] Abu Daawuud (227 na 4152). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (4152).
[6] Abu Daawuud (3755) na Ibn Maajah (3360). Nzuri k wa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (3755).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy (afk. 1250)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Hukm-ut-Taswwiyr, uk. 18-22
- Imechapishwa: 06/05/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy (afk. 1250)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Hukm-ut-Taswwiyr, uk. 18-22
Imechapishwa: 06/05/2026
https://firqatunnajia.com/02-mahali-asipoingia-malaika-wala-mtume/