2- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisimama wakati wa swalah ya faradhi na ya sunnah, akitekeleza maneno Yake (Ta´ala):
وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ
“Simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”[1]
Kuhusu safarini, alikuwa akiswali swalah za sunnah juu ya kipando chake.
Amewasunishia Ummah wake wakati wa khofu kubwa waswali kwa kutembea au kwa kupanda, kama ilivyotangulia. Hicho ndicho kilichozungumziwa katika maneno Yake (Ta´ala):
حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ
“Shikamaneni na swalah na swalah khaswa khaswa ya katikati na simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu. Mkihisi ukhofu basi [swalini na] huku mnatembea au mmepanda kipando, na mtakapokuwa katika amani mdhukuruni Allaah kama alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamyajui.”[2]
“Aliswali wakati wa maradhi ya mauti yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kukaa.” Ahmad na at-Tirmidhiy na ameisahihisha.
Aliswali mara nyingine kwa hali hiyo alipokuwa vibaya. Watu wakaswali nyuma yake kwa kusimama na akawaashiria wakae chini, ambapo wakawa wamekaa. Baada ya swalah akawaambia:
“Mmekaribia kufanya yale yanayofanywa na waajemi na warumi; wanawasimamia wafalme wao ilihali wao wamekaa. Msifanye hivo. Imamu ametengwa ili afuatwe. Hivyo akirukuu, nanyi rukuuni, akiinuka, nanyi rukuuni na endapo ataswali kwa kukaa, nanyi ikaeni. Muslim na wengineo. Imetajwa katika kitabu changu ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” chini ya Hadiyth 394.
[1] 02:138
[2] 02:238-239
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 77-78
- Marejeo: Firqatunnajia.com
- Imechapishwa: 08/10/2016

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 77-78
Marejeo: Firqatunnajia.com
Imechapishwa: 08/10/2016
https://firqatunnajia.com/02-kuswali-kwa-kusimama/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)