Kundi hili limedai kuwa Allaah ameridhia kule kutambua kwao. Ingelikuwa jambo na dini ya Allaah ni vile wanavosema watu hawa, basi kusingelikuwa na tofauti yoyote kati ya Uislamu na kile kipindi kabla ya kuja Uislamu. Wala kusingelikuwa na tofauti yoyote kati ya dini. Kwani Allaah anaridhia kwa wote hao yale madai yao ndani ya nyoyo zao pasi na kudhihirisha kuhitaji kutambua yale yaliyokuja na ujumbe wa kinabii na kujitenga mbali na mengine yote na kuachana na masanamu na waungu. Ikiwa mtu kama huyu ni muumini kisha mtu mwingine, ambaye moyo wake una utambuzi juu ya Allaah, akashuhudia ya kwamba Allaah ni wa pande mbili – kama wanavosema waabudia moto na mazanadiki – au mmoja katika utatu – kama wanavosema manaswara – akaswali kwa kuelekea msalaba na akaabudia moto, basi mtu mwenye ´Aqiydah hii angelilazimika kumtambua huyo mwingine kuwa na imani kamili kama imani ya Malaika na Mitume. Je, inawezekana kwa mtu ambaye anamjua Allaah na kukiamini Kitabu Chake na Mtume kusema kitu kama hicho? Kwa mujibu wetu hiyo ni kufuru ambayo hakuifikia hata Ibliys, sembuse wale makafiri wengine.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 27/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy