02. Hadiyth “Kuna saa mbili ambazo hufunguliwa milango ya mbingu… “

266 – Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ساعتان تُفتَح فيهما أبوابُ السماء، وقلّما تُرَدُّ على داعٍ دعوتُه؛ عند حضور النِّداةِ ، والصفِّ في سبيل الله

“Kuna saa mbili ambazo hufunguliwa milango ya mbingu. Ni mara chache du´aa itarudishwa du´aa ya mwombaji: pindi kunapokimiwa na katika safu katika njia ya Allaah.”[1]

Imekuja katika tamko jengine:

ثِنْتانِ لا تُرَدّان -أو قلّما يُردّان-: الدعاءُ عند النداءِ، وعند البأْسِ؛ حين يُلحِمُ بعضهم بعضاً

“Mambo mawili hayarudishwi, au ni mara chache yanarudishwa: du´aa wakati kunapokimiwa na wakati wa dhiki ambapo watu wanachinjana.”

Ameipokea Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” ambaye tamko lake limekuja:

“… wakati wa kuhudhuria swalah.”

Ameipokea al-Haakim na akaisahihisha na ameipokea Maalik kutoka kwa Swahabah.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/225-226)
  • Imechapishwa: 09/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy