267 – ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

:أنّ رجلاً قال: يا رسولَ الله! إنّ المؤذّنين يَفْضُلوننا؟ فقال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

.”قلْ كما يقولون، فإذا انتهيتَ فَسَلْ تُعْطَه”

“Bwana mmoja alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika waadhini wanatushinda ubora.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Semeni kama wanavosema. Mnapomaliza basi ombeni du´aa mtapewa kitu hicho.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa´iy na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” ambaye tamko lake linasema:

“Mnapomaliza basi ombeni du´aa mtapewa.”

Bi maana pasi na “kitu hicho”.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/226)
  • Imechapishwa: 09/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy