268 – ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) alisema wakati watu walimsema pindi alipojenga msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

:إنكم أكثرتُم ، وإنّي سمعتُ رسولَ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – يقول

مَن بنى مسجداً -[قال بُكير: حسِبتُ أنّه قال:] يبتغي به وجهَ الله-؛ بنى الله له بيتاً في الجنة

“Mmekithirisha. Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Yeyote atakayejenga msikiti [Bukayr amesema: “Nadhani alisema:] hali ya kuwa ni mwenye kukusudia uso wa Allaah, basi Allaah atamjengea nyumba Peponi.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

“… basi Allaah atamjengea mfano wake Peponi.”

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengineo.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Imechapishwa: 09/03/2022
  • taaliki: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/225-226)