02. Hadiyth “Hakika Ummah wangu wataitwa siku ya Qiyaamah… “

176 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakika Ummah wangu wataitwa siku ya Qiyaamah hali ya kuwa ni wenye mabaka na wenye kung´ara kutokana na athari ya wudhuu´. Hivyo basi, ambaye atakayeweza kurefusha mabaka yake basi na afanye hivo.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Imesemekana kwamba hayo maneno ya mwisho ni ya Abu Hurayrah, kitu ambacho kimetajwa na wanachuoni wengi[2] – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

Muslim amepokea kwa Abu Haazim aliyesema:

“Nilikuwa nimesimama nyuma ya Abu Hurayrah wakati ambapo alikuwa anatawadha kwa ajili ya kuswali. Alikuwa anatawadha mikono yake mpaka anafika kwenye makwapa. Nikasema: “Ee Abu Hurayrah, ni wudhuu´ aina gani huu?” Akasema: “Enyi kabila la Farruukh! Nyinyi mko hapa! Laiti ningelijua kuwa mko hapa basi nisingelitawadha kwa namna hii[3]. Nimemsikia kipenzi changu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Pambo ya muumini litafika pale ulipofika wudhuu´ wake.”

Ibn Khuzaymah amepokea katika “as-Swahiyh” yake kwa tamko mfano wa hilo, isipokuwa tu yeye amesema kwamba Abu Hurayrah ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Pambo litafika yale maeneo ya twahara.”

Bi maana yale mabangili na mapambo mengine watakayopambwa nayo watu wa Peponi.

[1] Swahiyh.

[2] Hayo pia ndio yamepitishwa na Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na mwanafunzi wake Haafidhw na Shaykh al-Naajiy.

[3] al-Qaadhwiy ´Iyaadhw amesema:

”Alichokuwa anamaanisha Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ni kwamba mwigizwaji anayefanya jambo katika hali ya dharurah, kutokana na wasiwasi au kutokana na maoni yasiyokuwa na nguvu hatakiwi kukifanya mbele ya watu wajinga wasiokuwa na elimu ili wasije kumwigiliza pasi na dharurah au wakadhani kuwa maoni yake dhaifu ndio ya lazima.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/185-186)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy