01. Hadiyth “Je, nikiyafanya hayo mimi nitakuwa muislamu?”

175 – Ibn ´Umar amepokea kutoka kwa baba yake (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema pindi Jibriyl alipomuuliza swali juu ya Uislamu:

“Uislamu ni kule kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kuhiji na kufanya ´umrah, kuoga kutokamana na janaba, kukamilisha wudhuu´ na kufunga Ramadhaan.” Akauliza: “Je, nikiyafanya hayo mimi nitakuwa muislamu?” Akajibu: “Ndio.” Akasema: “Umesema kweli.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. al-Bukhaariy, Muslim na wengineo wameipokea kwa tamko jengine lisilokuwa hili.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/185)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy