177 – Yeye pia amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifika makaburini akasema:

السَّلامُ عَلَيْكُمْ دارَ قومِ مؤمنين وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللهُ بكم عن قريبٍ لاحِقُونَ

“Amani ya Allaah iwe juu yenu, watu wa nyumba za waumini. Nasi – atakapo Allaah – karibuni tutaungana nanyi.”

Natamani laiti tungeliwaona ndugu zetu.” Wakasema: “Kwani sisi sio nduguzo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Nyinyi ni Maswahabah zangu[1]. Ndugu zangu ni wale ambao bado hawajakuja.” Wakasema: “Utawatambua vipi wale ambao hawajakuja kutoka katika Ummah wako, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Je, mtu hamtambui farasi wake mwenye mabaka na anayeng´aa aliye kati ya farasi weusi?” Wakasema: “Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Hakika wao watakuja wakiwa na mabaka na wenye kung´aa kutokana na wudhuu´ na mimi nitakuwa mwenye kuwatangulia katika Hodhi.”[2]

Ameipokea Muslim na wengineo.

[1] Haina maana kwamba wao sio ndugu zake, isipokuwa ni kwamba wao wamezidisha sifa nyingine ya kipekee; ambayo ni ya uswahaba. Hao wa mwanzo ni ndugu na Maswahabah, na wale ambao bado hawajakuja ni ndugu pekee na si Maswahabah. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

”Hakika si venginevyo waumini ni ndugu.” (49:10)

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/187)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy