02. Dalili ya kwanza kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

1- ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtum wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Muusa alikutana na Aadam na akasema: ”Wewe Allaah alikuumba kwa mikono Yake na akawaamrisha Malaika wakusujudie. Ninaapa kwa Allaah! Usingelifanya uloyafanya basi hakuna yeyote katika kizazi chako ambaye angeliingia Motoni.” Ndipo akasema: ”Ee Muusa! Wewe ndiye ambaye Allaah alikuchagua kwa ujumbe Wake na kukuzungumzisha… ”[1]

[1] Ibn Mandah katika ”Kitaab-ul-Iymaan” (11) na (13) na ad-Daaraqutwniy (207).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 13
  • Imechapishwa: 10/12/2018