01. Dalili kutoka katika Qur-aan juu ya mikono ya Allaah

Mkono wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni sifa ya Allaah miongoni mwa sifa Zake. Amesema (Ta´ala):

قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[1]

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

”Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa waliyoyasema. [Sivyo hivyo], bali mikono Yake imefumbuliwa hutoa atakavyo.”[2]

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ

”Je, hivi hawaoni kwamba Sisi tumewaumbia kutokana na vile viliyofanywa na mikono Yetu, wanyama hawa wanaowamiliki?”[3]

وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Mbingu zitakunjwa mkononi mwake mwa kuume.”[4]

يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ

”Mkono wa Allaah uko juu ya mikono yao.”[5]

[1] 38:75

[2] 05:64

[3] 36:71

[4] 39:67

[5] 48:10

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 13