03. Dalili ya pili kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

2- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Siku ya Qiyaamah Allaah atazikunja mbingu kisha atazishika kwa mkono Wake wa kuume na kusema: ”Mimi ndiye Mfalme! Wako wapi wenye jeuri?  Wako wapi wenye kiburi?”[1]

[1] Muslim (2148) na Abu Daawuud (4732).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 14
  • Imechapishwa: 10/12/2018