Kuhusu uongofu ambao una maana ya kujaaliwa ni kama mfano wa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ

”Hakika wewe huwezi kumwongoza umpendaye.”[1]

Huu ni uongofu wa kujaaliwa kuyafanyia kazi kimatendo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawezi kwa hali yoyote kumjaalia yeyote kufanya matendo mema. Angeliweza kuyafanya hayo basi angeliweza kumwongoza ami yake Abu Twaalib. Alijaribu naye mpaka akafikia kusema wakati wa kuaga kwake dunia:

“Ee ami yangu! Sema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`. Ni neno ambalo nitakutetea nalo mbele ya Allaah.”

Lakini limekwishatangulia neno mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) ya kwamba ni katika watu wa Peponi. Matokeo yake hakusema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`. Neno la mwisho akaishilia kusema:

“Yuko katika mila ya ´Abdul-Muttwalib.”[2]

Hata hivyo Allaah amemuidhinisha Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumfanyia uombezi, sio kwa sababu ni ami yake, lakini ni kwa sababu alimtetea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Uislamu. Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamfanyia uombezi na hivyo atakuwa katika adhabu ndogo ya Moto na huku amevaa viatu viwili ambavyo vinachemsha ubongo wake – na huyu ndiye mtu wa Motoni mwenye adhabu ya chini kabisa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kama isingelikuwa mimi basi angelikuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni.”

[1] 28:56

[2] al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 06-07
  • Imechapishwa: 05/03/2024