20 – ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Jaamiy´ bin Shaddaad, kutoka kwa al-Aswad bin Hilaal aliyesimulia kuwa Mu´aadh bin Jabal alisema kumwambia bwana mmoja:

“Keti nasi tuumini kitambo kidogo.”[1]

Bi maana tumtaje Allaah.

Sufyaan, al-Awzaa´iy na Anas walikuwa wakiamini hayo. Walikuwa wanaona kuwa matendo mema ya mtu yanazidisha Uislamu wa mtu, kwa sababu wote walikuwa wanaona kuwa matendo mema ni katika Uislamu. Dalili yao ya hilo ni yale ambayo Allaah (Ta´ala) amewasifu wale waumini katika maeneo matano ndani ya Qur-aan, ikiwa ni pamoja na:

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُواْ لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً

”Wale ambao waliambiwa na watu: “Hakika watu wamekusanyika dhidi yenu hivyo basi waogopeni”; yakawazidishia imani… ”[2]

وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا

“… na iwazidishie imani wale walioamini.”[3]

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ

“Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za waumini ili awazidishie imani pamoja na imani zao.”[4]

Sehemu zingine mbili tumekwishatangulia kuzitaja katika mlango wa kwanza. Ahl-us-Sunnah wakazifuata Aayah hizi na wakazifahamu kwa njia ya kwamba inazidi kutokana na matendo mema.

[1] Cheni ya wapokezi ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Abiy Shaybah ameipokea katika ”Kitaab-ul-Iymaan” (105) na (107) kupitia kwa al-A´mash, kutoka kwa Jaamiy´.

[2] 3:173

[3] 74:31

[4] 48:4

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 25/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy