Kuhusu maudhui ambayo tumekaa na kukusanyika kwa ajili yake ni kuhusu kuwasili kwa mwezi wa Ramadhaan. Kama mnavyojua, zimesalia siku na nyakati chache hadi kuingia kwa mwezi uliobarikiwa. Baada ya hapo mwezi utazuka kwa kheri zake zenye kuenea, neema zake za ukarimu na baraka zake zenye kufuatana.

Mwezi wa Ramadhaan umefika na ujio wake ni jambo kubwa kwa waislamu na athari kubwa katika nafsi zao. Kwa sababu wana shauku juu ya ujio wake, wanatazamia ujio wake, wanapeana bishara kwa kule kukaribia wake na wanafurahika furaha ilio kubwa pale inapoingia.  Wanafanya hivo kutokana na yale mema makubwa na sifa za kipekee wanazotambua kuhusu mwezi huu na msimu huu uliobarikiwa. Sifa ambazo zinaupambanua mwezi huu na kuutofautisha kati ya miezi iliyosalia.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 05
  • Imechapishwa: 02/04/2022