01. Muhimu kujua hukumu kuhusu Sujuud ya kusahau

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Himidi zote njema ni Zake Allaah, Mola wa viumbe. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad – ambaye kafikisha ujumbe wa wazi – na kizazi chake, Maswahabah zake na wale watakaomfuata kwa wema hadi siku ya Malipo.

Amma ba´d:

Hakika wengi miongoni mwa watu wanajahili hukumu nyingi zinazohusiana na Sujuud ya kusahau katika swalah. Miongoni mwao wako ambao wanaacha Sujuud ya kusahau mahali ambapo ni wajibu kusujudu. Na miongoni mwao wako ambao wanasujudu mahala ambapo sio pake. Na miongoni mwao wako ambao wanasujudu Sujuud ya kusahau kabla ya salamu ingawa mahali pake ni baada ya salamu. Na miongoni mwao wako ambao wanasujudu Sujuud ya kusahau baada ya salamu ilihali mahali pake ni baada ya salamu. Kwa ajili hiyo, ndio maana ikawa kujua hukumu zake ni jambo muhimu sana, na khaswa kwa maimamu ambao watu wanawafuata wao na wakabeba majukumu katika kufuata yale yaliyowekwa katika Shari´ah katika swalah zao ambazo wanawaongoza waislamu.

Kwa ajili hiyo, nikapendelea kuwaandikia ndugu zangu baadhi ya hukumu kuhusiana na mlango hali ya kuwa ni mwenye kutaraji kutoka kwa Allaah awanufaishe kwayo waja Wake waumini.

Nasema hali ya kuwa ni mwenye kutaka msaada kutoka kwa Allaah na nikitaraji kutoka Kwake atuongoze katika tawfiyq na usawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sujuud-us-Sahw, uk. 141
  • Imechapishwa: 07/04/2022