Mtu anahitaji subira katika hali tatu:

1- Kabla ya kuingia katika ´ibaadah kwa kusahihisha nia yake na Ikhlaasw na kuazimia kutelekeza maamrisho na kujiepusha na kujionyesha.

2- Wakati wa ´ibaadah kwa kulazimiana na subira na yale yote yanayoita katika mapungufu na uzembe. Wakati wa ´ibaadah anatakiwa kukumbuka nia yake na auhudhurishe moyo kwa Yule anayemuabudu. Mja anahitaji subira ili kuhakikisha nguzo, masharti, wajibu na mapendekezo ya matendo.

3- Subira baada ya kumaliza ´ibaadah ahakikishe anajiepusha na mambo yote yanayoiharibu ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ

“Enyi mlioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia.” 02:264

Kitu cha manufaa zaidi ambacho mja anaweza kufikia ni kuwa na subira kwa kuilinda ´ibaadah yake baada ya kumaliza kuitekeleza. Hii ndio maana ya maneno ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 143-144
  • Imechapishwa: 02/11/2016