Kuhusiana na madhambi na mambo ya uhalifu, mapokezi yamekaripia kwa sampuli nne:

1 – Madhambi yanayokanusha imani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, haibi mwenye kuiba pale anapoiba hali ya kuwa ni muumini.”[1]

“Si muumini yule ambaye hamsalimishi jirani yake na matatizo yake.”

“Imani inazuia mauaji. Muumini hauwi.”[2]

“Hakuna yeyote anayemwamini Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anayewachukia Wanusuraji.”[3]

“Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Hamtoamini mpaka mpendane.”[4]

Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Jihadharini na uwongo; kwani hakika inaiweka kando imani.”[5]

´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hana imani yule ambaye hana amana.”[6]

Sa´d amesema:

“Sifa zote ako nazo muumini isipokuwa khiyana na uwongo.”[7]

Ibn ´Umar amesema:

“Hakuna yeyote anayefikia uhakika wa imani mpaka aache mabishano, ijapo ni mwenye haki, na kuacha mzaha wa uwongo.”[8]

[1] al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Iymaan” (38) na (72).

[2] Abu Daawuud na al-Haakim kupitia kwa Abu Hurayrah, Abu Daawuud kupitia kwa Mu´aawiyah na Ahmad kupitia kwa az-Zubayr.

[3] Muslim.

[4] Muslim.

[5] Ahmad (1/5). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[6] Maneno haya yamesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Anas. Tazama ”al-Iymaan” (07) ya Ibn Abiy Shaybah.

[7] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kutoka kwa Swahabah. Imepokelewa pia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa cheni ya wapokezi dhaifu. Tazama ”al-Iymaan” (07) ya Ibn Abiy Shaybah.

[8] Sijayaona kutoka kwa Ibn ´Umar. Ameyapokea Ibn Abiy Ya´laa kutoka kwa baba yake na ´Umar kwa cheni ya wapokezi ambayo inatakiwa kutazamwa vyema. Tazama ”at-Targhiyb wat-Tarhiyb” (4/28). Ahmad ameipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 67-70
  • Imechapishwa: 27/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy