Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

MAELEZO

Kwa jina la Allaah – Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ameanza kitabu chake kwa jina la Allaah kwa kuiga Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) kilichoanzwa kwa Basmalah. Kadhalika amefanya hivo kwa kufuata Hadiyth isemayo:

”Kila jambo lililo na umuhimu lisiloanzwa kwa Jina la Allaah, basi limeondoshewa baraka.”[1]

Vilevile amemuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuwa siku zote akianza barua zake kwa jina la Allaah.

Mwingi wa rehma [ar-Rahmaan] – Mwingi wa rehma ni katika majina maalum ya Allaah (´Azza wa Jall) na hivyo haliitwi mtu mwingine. Mwingi wa rehma maana yake ni Yule Mwenye kusifika na rehma kunjufu.

Allaah – Ni jina la Allaah (Jalla wa ´Alaa) pekee ambalo linafuatiwa na majina mengine yote. Allaah (Ta´ala) Amesema:

الر كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ  اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَوَيْلٌ لِلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ

 “Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu katika viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Allaah ambaye ni Vyake pekee vyote viliyomo katika mbingu na katika ardhi. Na ole kwa makafiri kutokana na adhabu kali.” (Ibraahiym 14:01-02)

Hatusemi kuwa neno la kitukufu ”Allaah” ni sifa, isipokuwa hali ya kubainisha. Neno la kitukufu linakuwa na maana ya sifa yenye kufuata kwa kile kinachosifiwa.

Mwingi wa rehema [ar-Rahmaan] – Mwingi wa rehema ni katika majina maalum ya Allaah (´Azza wa Jall) na hivyo haliitwi mwingine. Mwingi wa rehema maana yake ni Yule mwenye kusifika na rehema kunjufu.

Mwenye kurehemu [ar-Rahiym] – Ni jina ambalo huitwa Allaah (´Azza wa Jall) na wengineo. Maana yake ni mwenye rehema zenye kuendelea. Mwingi wa rehema maana yake ni Mwenye rehema zenye kuenea, na Mwenye kurehemu, ambaye ni mwenye rehema zenye kuendelea, yakikusanywa, basi maana yake inakuwa “Mwingi wa rehema anayemfikishia rehema Zake kwa anayemtaka katika waja Wake”. Allaah (Ta´ala) Amesema:

يُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ وَيَرْحَمُ مَنْ يَشَاءُ وَإِلَيْهِ تُقْلَبُونَ

“Anamuadhibu amtakaye na anamrehemu amtakaye na Kwake mtarudishwa.” (al-´Ankabuut 29:21)

[1] as-Suyuutwiy ameiegemeza katika ”al-Jaamiy´-us-Swaghiyr” (04/147) ya ar-Rahaawiy na ameipokea pia al-Khattwaabiy katika “al-Jaamiy´” (02/69).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 16-18
  • Imechapishwa: 10/05/2020