Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Tambua – Allaah Akurehemu – ya kwamba ni wajibu juu yetu kujifunza masuala mane:

MAELEZO

Ujuzi – Kuwa na utambuzi wa kitu kama jinsi kilivyo kwa njia ya kihakika. Utambuzi huu una daraja sita:

1- Ujuzi: Wa kukitambua kitu kama jinsi kilivyo kikweli kwa njia ya kihakika.

2- Ujinga mwepesi: Wa kutokuwa na utambuzi kabisa.

3- Ujinga wa uliyopandiana. nao ni kule kukitambua kitu kwa njia inayoenda kinyume na uhakika wake.

4- Ufikiriaji: Ambao ni kukitambua kitu wakati kinyume chake pengine ndio ikawa sahihi zaidi.

5- Mashaka: Ambayo ni kule kukitambua kitu pamoja na uwezekano wa kuwepo kitu kingine kinachoweza kuwa kama kile.

6- Dhana: Ambayo ni kule kukitambua kitu na wakati huohuo kuna uwezekano kikawa ni sahihi zaidi kuliko kile kinachoenda kinyume.

Ujuzi umegawanyika sehemu mbili; ya kidharurah na kinadhari.

Kuhusu ujuzi wa kidharurah, ni ule ambao kuyatambua mambo kidharurah ni jambo la wajibu kwa njia ya kwamba mtu hahitajii kufanya utafiti wala dalili. Mfano wa hilo ni mtu kujua kuwa moto unachoma.

Kuhusiana na ujuzi wa aina ya kinadhari, ni ule ambao unahitajia nadhariya na dalili. Katika mfano wa ujuzi huu ni kama mtu kujua kwamba ni wajibu kutia nia katika Wudhuu.

Allaah akurehemu – Allaah akumiminie rehema Zake ambazo unafikia malengo yako na kukuokoa na yawezayo kukudhuru. Maana ya hilo ni Allaah akusamehe yaliyopita katika madhambi yako na akuwafikishe na kukuhifadhi na yaliyo huko mbeleni. Maana hii ni pale endapo rehema inapotajwa peke yake. Ama pale ambapo inapoambatanishwa pamoja na msamaha, msamaha unakuwa kwa yale madhambi yaliyopita, wakati rehema na Tawfiyq inakuwa katika kheri na kusalimika na madhambi siku za mbeleni.

Kitendo cha mwandishi (Rahimahu Allaah) kinajulisha jinsi anavyomtilia umuhimu, kumuonea huruma yule anayemzungumzisha na kumtakia kheri zote.

Masuala haya ambayo mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ameyataja yanaizunguka dini yote. Kwa hiyo, yanapaswa kutiliwa umuhimu mkubwa kutokana na manufaa yake makubwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 10/05/2020