Adhkaar wakati wa kulala
55 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Atapofika mmoja wenu kitandani mwake basi akikungute kitanda kwa shuka yake mara tatu na aseme:
بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فَاغْفِرْ لَهَا، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين
”Kwa jina lako, Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili Yako nitaunyanyua. Ukiizuia roho yangu, basi isamehe, na ukiirejesha, basi ihifadhi kwa yale unachowahifadhi kwayo waja Wako wema.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Katika tamko la Muslim imekuja:
”Atakapoenda mmoja wenu kitandani mwake basi akikungute kitanda kwa ncha ya izari yake na amtaje Allaah, kwani hajui kilicho kuja baada yake kitandani mwake. Na akitaka kulala, basi alalie ubavu wake wa kulia na aseme:
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبِّي ، بِكَ وَضَعْتُ جَنْبِي، وَبِكَ أَرْفَعُهُ ، إِنْ أَمْسَكْتَ نَفْسِي فَاغْفِرْ لَهَا، وَإِنْ أَرْسَلْتَهَا فَاحْفَظْهَا بِمَا تَحْفَظُ بِهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِينَ
”Utakasifu kutokana na mapungufu ni Wako, Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili Yako nitaunyanyua. Ukiizuia roho yangu, basi isamehe, na ukiirejesha, basi ihifadhi kwa yale unachowahifadhi kwayo waja Wako wema.”
MAELEZO
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Atakapoenda mmoja wenu kitandani mwake… ”
Aikungute kwa ncha ya nguo yake mara tatu. Kitendo cha kukunguta kitanda kinafikiwa kwa kutumia ncha ya nguo, kutikisa kitanda au kutikisa shuka ilio juu yake. Shaykh wetu muheshimiwa ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) ameonelea hivo. Kinachotilia nguvu hayo ni ubainifu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa hekima ya kuikunguta.

“… kwani hajui kilicho kuja baada yake kitandani mwake.”
Pengine kumekuja baadhi ya wadudu wenye madhara na vitu vyenye sumu. Kufanya hivo ni kwa njia ya mapendekezo. Kisha baada ya hapo alale kwa ubavu wake wa kulia. Kisha aseme Dhikr hii.

“Ukiizuia roho yangu, basi isamehe.”
Bi maana ukiifisha irehemu na uisamehe. Inaweza mtu kuchukuliwa roho yake akiwa ndani ya usingizi. Amesema (Ta´ala):
اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى
“Allaah anazifisha nafsi wakati wa kufa kwake na zile zisizokufa katika usingizi wake. Huzizuia zile ambazo amezihukumia mauti na huzituma nyingine mpaka katika muda maalumu uliopangwa.”[2]

”Na ukiirejesha, basi ihifadhi kwa yale… ”
Ukiibakiza basi ihifadhi kutokana na shari na fitina kwa yale ambayo unawahifadhi kwayo waja Wako wema.
[1] al-Bukhaariy (7393) na Muslim (2714).
[2] 39:42
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 65-66
- Imechapishwa: 20/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 65-66
Imechapishwa: 20/10/2025
https://firqatunnajia.com/01-kukunguta-kitanda-wakati-wa-kulala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket