15. Du´aa ya kumuomba Allaah authibitishe moyo wako katika dini Yake

54 – ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ القُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا علَى طَاعَتِكَ

“Ee Allaah! Mwenye kuzipindua nyoyo, Upindue moyo wangu katika utiifu Wako.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hapa kuna fadhilah za du´aa hii:

اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ القُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا علَى طَاعَتِكَ

“Ee Allaah! Mwenye kuzipindua nyoyo, Upindue moyo wangu katika utiifu Wako.”

Hadiyth nyingine Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Du´aa yake alikuwa akiomba kwa wingi ilikuwa:

يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ

“Ee Mwenye kuzipindua nyoyo, Uthibitishe moyo wangu katika dini yako.”

Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni kwa wingi uliyoje unaomba:

يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ

“Ee Mwenye kuzipindua nyoyo, Uthibitishe moyo wangu katika dini yako?”

Akasema: “Ee Umm Salamah! Hakuna mwanadamu yeyote isipokuwa moyo wake uko kati ya vidole viwili katika vidole vya Allaah; Anaoutaka anaunyoosha na Anaoutaka anaupindisha.”[2]

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaomba hivi licha ya kwamba ndiye bwana wa viumbe. Kwa hiyo inampasa muislamu aomba kwa wingi du´aa hii.

[1] Muslim (2654).

[2] at-Tirmidhiy (3522).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 61
  • Imechapishwa: 20/10/2025