56 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinipa kazi ya kuchunga zakaah ya Ramadhaan. Nikajiliwa na mwenye kuja na kuanza kuchukua chakula ambapo nikamkamata na kumwambia: “Nitakupeleka kwa Mtume wa Allaah…. Akamwambia: “Unapoenda kulala mwako, basi soma Aayaah al-Kursiy. Utaendelea kuhifadhiwa na Allaah na hutokaribiwa na shaytwaan mpaka kupambazuke. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Amesema kweli ijapo ni mwongo. Huyo alikuwa ni shaytwaan.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Hadiyth hii inafahamisha kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kusoma Aayah al-Kursiy wakati wa kulala na kwamba ni miongoni mwa sababu za Allaah (´Azza wa Jall) kumuhifadhi mja kutokana na shaytwaan.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Utaendelea kuhifadhiwa na Allaah… “

Haya ni maneno ya shaytwaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akayakubali na kusema:

“Amesema kweli ijapo ni mwongo. Huyo alikuwa ni shaytwaan.”

Hukumu inachukuliwa baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumsadikisha.

[1] al-Bukhaariy (3275).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 20/10/2025