03. Kusoma al-Ikhlaasw, an-Falaq an-Naas wakati wa kulala

57 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaenda kulala hukusanya viganja vyake, akasoma al-Ikhlaasw, an-Falaq an-Naas na akifuta kwavyo mwili wake.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

al-Ikhlaasw kunakusudiwa:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ

“Sema: “Allaah ni Mmoja pekee… “

na:

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَق

“Sema: “Najilinda na Mola wa mapambazuko.. “

na:

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

“Sema: “Najilinda na Mola wa watu… “

Hapa kuna dalili ya kwamba ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuomba kinga na kusoma wakati wa kulala. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikusanya viganja vyake na akitema cheche za mate ndani yake na akisoma Suurah hizi. Baada ya hapo anafuta kwayo uso wake, kichwa chake na sehemu atayoweza katika mwili wake. Kisha anarudia kufanya hivo mara ya pili na mara ya tatu, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth nyingine[2].

[1] al-Bukhaariy (6319).

[2] Ahmad (06/116) na al-Bukhaariy (5018).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 67
  • Imechapishwa: 20/10/2025