Swali: Najua kuwa furaha ya kweli ipo katika kumcha Allaah na kuipa nyongo dunia hii. Nataka kuwa mnyenyekevu katika chakula changu, nguo zangu, kinywaji changu na kipando changu, lakini siwezi kwa sababu ya hali ya starehe tuliyonayo katika maisha ya sasa. Ni zipi nasaha zako?
Jibu: Nasaha yetu kwako ni kwamba usijitese wala kujikalifisha, bali kuwa katikati. Usifanye jambo litakalokufanya udharauliwe, kama kuvaa nguo duni zisizokufaa. Vivyo hivyo katika chakula; uwe katikati katika mambo yako. Usijifanye kama masikini ilihali wewe ni tajiri wala usijifanye kama matajiri ilihali wewe ni masikini. Fanya kwa kiwasngo cha uwezo wako. Allaah anapenda kuona athari ya neema Yake juu ya mja Wake. Hivyo basi ikiwa Allaah amekufungulia, basi kula na vaa kwa wastani bila kujikalifisha na bila kukanusha neema za Allaah. Angalia wale walio chini yako, usiwaangalie walioko juu yako ili usidharau neema za Allaah juu yako. Ama kujikalifisha katika mavazi, vinywaji na vyakula, haifai. Mwanadamu anatakiwa aangalie wastani wa watu mfano wake katika mavazi na chakula ili asidharau neema za Allaah juu yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31329/ما-النصيحة-لتوازن-المسلم-بين-الترف-والتقتير
- Imechapishwa: 20/10/2025
Swali: Najua kuwa furaha ya kweli ipo katika kumcha Allaah na kuipa nyongo dunia hii. Nataka kuwa mnyenyekevu katika chakula changu, nguo zangu, kinywaji changu na kipando changu, lakini siwezi kwa sababu ya hali ya starehe tuliyonayo katika maisha ya sasa. Ni zipi nasaha zako?
Jibu: Nasaha yetu kwako ni kwamba usijitese wala kujikalifisha, bali kuwa katikati. Usifanye jambo litakalokufanya udharauliwe, kama kuvaa nguo duni zisizokufaa. Vivyo hivyo katika chakula; uwe katikati katika mambo yako. Usijifanye kama masikini ilihali wewe ni tajiri wala usijifanye kama matajiri ilihali wewe ni masikini. Fanya kwa kiwasngo cha uwezo wako. Allaah anapenda kuona athari ya neema Yake juu ya mja Wake. Hivyo basi ikiwa Allaah amekufungulia, basi kula na vaa kwa wastani bila kujikalifisha na bila kukanusha neema za Allaah. Angalia wale walio chini yako, usiwaangalie walioko juu yako ili usidharau neema za Allaah juu yako. Ama kujikalifisha katika mavazi, vinywaji na vyakula, haifai. Mwanadamu anatakiwa aangalie wastani wa watu mfano wake katika mavazi na chakula ili asidharau neema za Allaah juu yake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31329/ما-النصيحة-لتوازن-المسلم-بين-الترف-والتقتير
Imechapishwa: 20/10/2025
https://firqatunnajia.com/ishi-maisha-ya-wastani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket